Uchaguzi S/Mitaa: Watanzania wanaamua

Zoezi hilo lililoanza mapema saa mbili asubuhi kwa saa za afrika mashariki litaendelea hadi saa 12 jioni.

DAR ES SALAAM – Zoezi la upigaji kura limeanza rasmi nchini Tanzania ambapo wananchi waliojiandikisha wanashiriki kuchagua Wenyeviti, Wajumbe Wanawake na Wajumbe Mchanganyiko wa serikali za mitaa.

Zoezi hilo lililoanza mapema saa mbili asubuhi kwa saa za afrika mashariki litaendelea hadi saa 12 jioni.

Shughuli za kawaida katika maeneo mengi katika Jiji la Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya ambapo timu yetu ya wanahabari imepiga kambi zinaonekana kusimama. Maduka mengi yamefungwa.

Advertisement

Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa leo itakuwa siku ya mapumziko kwa wakazi wa Tanzania Bara kuruhusu washiriki zoezi muhimu la uchaguzi wa serikali za mitaa.