ETHIOPIA – Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika anapaswa kupata uungwaji mkono wa angalau mataifa 33 ili kushinda kiti hicho.
Uchaguzi huu unaweza kuchukua hadi duru tatu iwapo kizingiti hakitafikiwa katika duru ya kwanza ya upigaji kura.
Katika duru ya kwanza—ambayo kwa kawaida hufanyika kwa kura ya siri—wagombea wote hujumuishwa kwenye karatasi ya kura.
Iwapo hakuna mgombea anayefanikisha kupata kura 33 kati ya mataifa 48 shiriki kufikia duru ya tatu, karatasi ya kura itapunguzwa na kubaki na wagombea wawili wa juu. Faki alichaguliwa katika duru ya saba kwa kura 38, akipita kizingiti kinachohitajika.
Kenya ilipata changamoto kushawishi uungwaji mkono kutoka kwa majirani wake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwemo Tanzania, Uganda na Burundi.
Mwaka huu, mataifa saba hayatahusika katika kura hiyo kufuatia kusimamishwa kwao kutokana na kukosa utawala wa kikatiba. Mataifa hayo ni Burkina Faso, Chad, Gabon, Guinea, Mali, Sudan na Niger.
Uchaguzi wa 2025 umepangwa kufanyika wakati wa Mkutano wa 38 wa AU huko Addis Ababa, Ethiopia.
Wagombea wakuu ni Raila Odinga (Kenya), Mahmoud Ali Youssouf (Djibouti), na Richard Randriamandrato (Madagascar).
Wanaowania nafasi ya naibu mwenyekiti wa AUC ni Salah Francis (Algeria), Selma Malika (Algeria), Mohamed Fathi (Misri), Hana Morsy (Misri), Najat Elhajjaji (Libya) na Latifa Akharbach (Moroko).
Upigaji kura utaanza kwa uchaguzi wa mwenyekiti wa tume, ukifuatiwa na wa naibu mwenyekiti. Baada ya hapo, bunge litateua makamishna walioteuliwa na Baraza Kuu la AU kusimamia uchaguzi wa mwenyekiti.
Uchaguzi huu unafuata kanuni ya mzunguko wa kikanda, ikihakikisha uwakilishi wa haki katika kanda tano za Afrika: Mashariki, Kaskazini, Kati, Kusini na Magharibi.
Kwa uchaguzi wa 2025, Kanda ya Mashariki imeteua wagombea wa uenyekiti, huku Kanda ya Kaskazini ikitoa wagombea wa nafasi ya naibu mwenyekiti.
PIA SOMA: Samia kuongoza ajenda nishati safi AU
Kwa manaibu wa AUC, kila kanda lazima itoe wagombea wa kiume na wa kike ili kukuza usawa wa kijinsia.
Mwenyekiti na naibu wake hawawezi kutoka kanda moja, ili kuhakikisha uwakilishi wa utofauti. Wana hudumu kwa kipindi cha miaka minne, kinachoweza kurefushwa mara moja.
Endapo hakuna mgombea anayefanikisha kupata thuluthi mbili ya kura baada ya duru tatu, mgombea mwenye kura chache atalazimika kujiondoa.
View this post on Instagram
Mgombea aliyebaki lazima apate idadi inayohitajika la sivyo uchaguzi utasimamishwa na naibu mwenyekiti atachukua uongozi kwa muda.
Katika uchaguzi wa mwenyekiti wa AUC, upigaji kura huendelea hadi mgombea mmoja apate thuluthi mbili ya kura.
Endapo wagombea ni wawili pekee na hakuna anayefanikisha thuluthi mbili, mgombea mwenye kura chache atajiondoa.
Iwapo mgombea mmoja pekee yupo na hashindi thuluthi mbili kufikia duru ya tatu, mwenyekiti atasitisha upigaji kura.
Katika hali kama hiyo, naibu mwenyekiti atachukua nafasi ya uenyekiti wa tume hadi uchaguzi mpya ufanyike.
Iwapo mkwamo huu utahusu nafasi ya naibu mwenyekiti, kamishna mwandamizi zaidi atateuliwa kuchukua nafasi hiyo kwa muda hadi uchaguzi mpya ufanyike.
Mwaka 2017, Amina Mohamed wa Kenya alipata kura 16 katika duru ya kwanza dhidi ya kura 14 za Moussa Faki, huku kura zilizosalia zikigawanyika kati ya wagombea wengine.