DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza eneo la biashara ambalo ghorofa lilianguka Novemba 16, Kariakoo Dar es Salaam, lifungwe na kusiwe na biashara yoyote wakati taratibu za kukarabati eneo hilo zikiendelea.
Rais ametoa agizo hilo leo Novemba 20 alipozungumza na wananchi waliojitokeza eneo hilo, huku akisisitiza kuwa baada ya kukarabati eneo hilo shughuli za biashara zitaendelea.
“Kwa eneo hili ambalo kuna hatari na maeneo ya jirani, uchochoro wote huu ningeomba ufungwe, ilI watalamu wawepo kazi ya kufukuwa jengo iendelee, na watu wasiwe karibu,” amesema Rais Samia.
Akizungumza katika eneo hilo, kiongozi huyo amesema kwa maeneo ambayo hatari iko mbali wafanyabiashara wanaweza kuendelea na biashara zao.