SUDAN: MWAKILISHI wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya haki za binadamu,Tom Fletcher ameonyesha wasiwasi wake kuhusu vitendo vya udhalilishaji wa kingono vinavyoendelea kufanywa dhidi ya wanawake wa Sudan.
Akizungumza katika ziara yake ya kwanza katika mji wa Port Sudan, Fletcher ambaye anaongoza Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kiutu (OCHA), amesema anahisi aibu kwa kushindwa kuwalinda wanawake wa Sudan ambao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Katika ziara yake nchini Sudan, Fletcher amekutana na mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan ambapo wamejadili kuhusu masuala ya kupeleka misaada katika maeneo ya migogoro.
Mwezi uliopita ujumbe huo ulirekodi kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji,unyanyasaji wa kingono na utekaji nyara kwa madhumuni ya kingono pamoja na madai ya kulazimishwa ndoa na biashara haramu ya binadamu.