ETHIOPIA : Imeelezwa kuwa mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya Shirikisho vya Ethiopia na wanamgambo kaskazini mwa magharibi nchini humo yanaweza kuleta athari kwa wakimbizi wanaotoka Sudan.
Haya yamesemwa na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, lenye makao yake huko New York, Marekani.
Naibu Mkurugenzi wa Human Rights Watch barani Afrika Laetitia Bader amesema wakimbizi wa Sudan nchini Ethiopia wamekuwa wakidhalilishwa na makundi tofauti ya wanamgambo waliojihami kwa zaidi ya mwaka sasa.
Ripoti hiyo imesema watu ambao waliojihami wamefanya mauaji, uporaji, utekaji nyara na kudai kulipwa pesa ili kuwaachia huru, na kuwafanyisha wakimbizi kazi za lazima karibu na kambi hizo.
Hatahivyo Shirika hilo limetuma matokeo yake ya awali ya ripoti hiyo kwa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Ethiopia na kukiri kambi hizo ziko karibu na maeneo yenye machafuko lakini wakimbizi wa Sudan wako salama.