Udumavu wafikia asilimia 35 Ruvuma

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas amesema udumavu bado changamoto ambapo takwimu zinaonesha mkoa huo una udumavu kwa asilimia 35.6.

Kanali Thomas amesema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa utekelezaji wa mkataba wa lishe uliofanyika katika ukumbi wa Chandamali Manispaa ya Songea.

Amewaagiza waganga wakuu wa wilaya kuendelea kusimamia utekelezaji wa masuala ya lishe katika afua mbalimbali kuanzia ngazi ya jamii,vituo vya tiba, ngazi ya kata,vijiji na mitaa.

Advertisement

“Bado hatufanyi vizuri katika eneo la udumavu,Mkoa wetu udumavu ni asilimia 35.6,hivyo lazima mtambue kuwa bado tuna kazi kubwa ya kusimamia afua za lishe katika ngazi ya jamii na vituo vya kutolea huduma za afya’’,alisisitiza.

Amewaagiza wakuu wa shule kuhakikisha kila shule inatoa huduma ya chakula kwa uhakika kwa wanafunzi wote badala ya kutoa chakula kwa madarasa ya mitihani yakiwemo darasa la nne, kidato cha pili na cha nne huku madarasa mengine yakipata chakula kwa idadi ndogo.

Mikoa yenye mitano yenye kiwango kikubwa cha udumavu nchini ni pamoja na Iringa inayoongoza kwa asilimia 56.6,Njombe asilimia 50.4,Rukwa asilimia 49.8,Geita asilimia 38.6 na Ruvuma asilimia 35.6