Uhaba wa vitunguu wapaisha bei

UHABA wa vitunguu katika soko la Ilala jijini Dar es Salaam, umesababisha bei ya vitunguu kuwa juu na kufikia kati ya Sh 350,000 na Sh 360,000 kwa gunia.

Mwenyekiti wa Wauza Vitunguu katika soko hilo, Ally Mbiku ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na HabariLEO.

Amesema ongezeko hilo limesababishwa na kutegemea zaidi vitunguu vingi kutoka mkoani Arusha, kwa kuwa mkoani Iringa mwaka huu hakukuwa na mavuno mzuri.

Amesema endapo kunakuwa hakuna uhaba wa zao hilo, miezi kama hii bei kwa gunia inakuwa ni kati ya Sh 70,000 na Sh 80,000.

Amesema kwa siku magunia kati ya 50 hadi 100 ya vitunguu hushushwa sokoni hapo, ingawa kuna wakati kwa siku moja moja hufikia gunia 200.

Amesema wateja wao huchukua kwa jumla na kuenda kuuza rejareja.

Habari Zifananazo

Back to top button