HAITI : ZAIDI ya watu 700,000 wameyakimbia makazi yao nchini Haiti na nusu yao wakiwa ni watoto, kutokana na kuongezeka kwa machafuko ya magenge ya uhalifu.
Shirika la Wahamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) limesema karibu watu 702,973 washayakimbia makazi yao.
Hatahivyo, wamesema idadi ya wakimbizi nchini humo imeongezeka kwa asilimia 22 ambao wakimbizi wa ndani tangu mwezi Juni mwaka huu.
SOMA: Kikosi kutumwa Haiti kutuliza ghasia
Kutokana na machafuko haya, Shirika hili limetoa ombi maalum kwa Jumuiya za Kimataifa kuanza kulijadili na kuliangalia kwa ukaribu ili kuepusha madhara mengine makubwa nchini humo.