UINGEREZA : MAMIA ya safari za ndege zimefutwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow, Uingereza, baada ya moto uliozuka katika kituo cha kupoza umeme kusababisha kukatika kwa nishati kwenye uwanja huo.
Hitilafu hiyo imesababisha matatizo kwa maelfu ya abiria, ambapo ndege nyingi zimekwama kutua au kuruka. Kwa mujibu wa mtandao wa kufuatilia safari za ndege wa FlightRadar, karibu ndege 1,350 zimeathirika na hitilafu hiyo.
Mashirika ya ndege kadhaa yamelazimika kuwapeleka abiria waliotarajiwa kuwasili au kuunganisha safari kupitia Heathrow kwenye viwanja vingine vya ndege barani Ulaya.
Mamlaka za uwanja huo zimesema kuwa bado hawana uhakika kuhusu muda utakaotumika kurejesha umeme, jambo ambalo linaweza kuendelea kuvuruga safari za abiria.
SOMA: Marubani ATCL kufundisha, kusimamia ndege Nigeria