Ujenzi Bandari ya Bagamoyo waiva

DAR ES SALAAM; MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesaini hati ya makubaliano na Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL) Tanzania Ltd yenye makao makuu yake Ufaransa kwa ajili ya usanifu, ujenzi na uendeshaji wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo.
Hati hii ya makubaliano imesainiwa jana katika makao makuu ya TPA, Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa na Rais wa AGL ambayo ni kampuni tanzu ya MSC, Philippe Labonne.
Mbossa amesema kusainiwa kwa hati ya makubaliano ni ishara ya utayari wa kuanza kwa mradi wa bandari mpya ya Bagamoyo ambapo kwa kuanzia, AGL itaanza usanifu na ujenzi wa gati tatu mpya za kisasa kati ya 28 zinazotarajiwa kujengwa katika bandari hiyo pamoja na gati mbili mpya za kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam.
“Tunategemea kuanza ujenzi wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo mapema Januari na pia tunawakaribisha wawekezaji wengine wa ndani na wa nje katika mradi huo ambao lengo ni kuleta mapinduzi makubwa katika shughuli za kibandari nchini,” alisema Mbossa.
Kwa upande wake, Labonne alisema wameamua kuingia makubaliano na TPA na kuwekeza Tanzania kutokana na kuwa nchi yenye amani, usalama na mazingira bora na tulivu ya uwekezaji. Alisema ni sehemu sahihi kijiografia kwa sekta ya uchukuzi na ni lango la biashara kitaifa na kimataifa.
“Naamini Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi kimaendeleo, ikiwa na mtaji mkubwa wa watu na mtazamo chanya na pia, ni lango la kuingilia nchi nyingi Afrika na kuyafikia masoko ya kimataifa,” alisema. Aliendelea: “Naamini ushirikiano huu utafungua mambo mengi, ikiwemo kutengeneza ajira ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa,” alisema.
Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa gati mpya tatu utajengwa kwa miaka mitatu na AGL imepata nafasi hii ya kushirikiana na TPA katika ujenzi huo, kutokana na uzoefu wao kama kampuni kubwa ya huduma za usafirishaji na lojistiki.
Inatoa huduma kamili za usafirishaji, usimamizi wa mizigo, usafirishaji wa kimataifa na huduma za forodha, ikihudumia sekta mbalimbali kama uchimbaji, mafuta, chakula na misaada ya kibinadamu, ikiwa sehemu ya kundi la kimataifa la AGL (zamani Bolloré T&L) na sasa wakiwa chini ya MSC.




Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com