Ujenzi barabara uende na uwekaji taa -Ulega

KILIMANJARO: Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemuelekeza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha anamsimamia Mkandarasi, Kings Builder kukamilisha ujenzi wa madaraja saba ya dharura katika eneo la Kileo lililopo barabara kuu ya Himo Junction – Same ukamilike kulingana na muda wa mkataba uliopangwa.
Ameelekeza ujenzi huo uende sambamba na uwekaji wa taa za barabarani, njia za wananchi kuelekea kwenye makazi yao, vituo vya mabasi na bodaboda pamoja na kuelekeza maji ya Mto Ng’ona kwenye njia yake.

Ulega ametoa maelekezo hayo Novemba 29, 2025 alipokuwa akikagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa mradi huo ambao umefikia asilimia 70 ya utekelezaji wake.
Ameeleza kuwa ni dhamira ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanafanya kazi usiku na mchana kwa lengo la kuijenga nchi yao hivyo ni muhimu eneo hilo kufungwa taakwa ajili ya biashara na usalama.
“Hakikisha unatafuta taa zisipungue 15 hadi 20 zifungwe katika eneo hili”, amesisitiza Ulega.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameeeleza kuwa tayari ofisi yake imefanya mazungumzo na TPC kwa ajili ya kupata mitambo ya kusaidia kuelekeza maji ya Mto Ng’ona katika njia yake na muda wowote kuanzia sasa wataanza zoezi hilo kabla ya mvua hazijaanza wakishirikina na Uongozi wa Kata hiyo pamoja na wazee wanaoufahamu asili ya mto huo.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Motta Kyando ameahidi mbele ya Waziri Ulega kushughulikia suala la taa za barabarani, kituo cha bodaboda, kituo cha basi katika eneo la Kileo na Hedaru Wilayani Same pamoja na njia za wapita kwa miguu kuelekea makazi ya watu.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Enock Koola amemuomba Waziri Ulega kuitupia jicho ujenzi wa barabara ya Kilema Pofu – Mandaka ili iweze kukamilika kwa kiwango cha lami na hivyo kuchochea maendeleo ya Sekta ya utalii na uchumi wa Moshi.

Mradi huo wa dharura unahusisha ujenzi wa madaraja 7 na barabara za maungio zenye urefu wa mita 1,600 ambao unatekelezwa na Mkandarasi Kings Builders na kusimamiwa na Kitengo cha TECU kwa gharama ya Sh bilioni 6.8 na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2025.




I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com