MENEJA wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage amesema ujenzi wa barabara ya Tamco-Mapinga yenye urefu wa kilometa 14 unatarajia kuanza hivi karibuni.
Mhandisi Mwambage amebainisha hayo wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara kilifanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani, mjini Kibaha ambapo alisema hatua za awali za ujenzi huo zimeanza baada ya kibali kutolewa Februari mwaka huu.
Alisema ujenzi wa barabara hiyo ni hatua kubwa na muhimu ya maendeleo ambapo utarahisisha usafiri kwa wananchi wanaoenda Bagamoyo na Bunju ambapo Kwa sasa wanalazimika kuzunguka kupitia Mbezi na Tegeta.
“Ujenzi wa barabara hii muhimu utaanza mapema na tayari maandalizi yamekamilika lakini pia usanifu unaendelea kufanywa kupata gharama halisi za ujenzi wa barabara ynhingine ya Chalinze Utete yanye urefu wa kilometa 354.
9 .
Aidha alisema ujenzi wa barabara ya Chalinze Utete utarahisisha kufika mikoa ya Kusini kupitia Chalinze lakini pia kwa wanaoenda Bwawa la Mwalimu Nyerere wakitokea Chalinze watapunguza mzunguko iwapo ikikamilika
Awali katika kikao hicho mhandisi Mwambage akiwasilisha makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025, alisema jumala ya Sh. 18.9 billion zimetegwa Kwa ajili ha matengenezo ya ya barabara sambamba na Sh. 19.4 bilion kwa ajili ya Maendeleo.
“Serikali imeendelea kitenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ha mayengenezo ya barabara zetu pamoja na maendeleo lakini changamoto inayotukabili ni vitendo vya baadhi ya wananchi kuendelea kusogea kwenye hifadhi ya barabara na kufanya shughuli za kibinadamu,”alisema
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, alisema aliwataka Wakala wa Barabara nchini TANROADS pamoja na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA, kujijengea utaratibu wa kufanya maombi ya fedha kwa wakati hatua itakayosaidia kukamilika kwa miradi ya barabara kwa wakati.