Ujenzi SGR Tanga-Arusha-Musoma wahojiwa bungeni

DODOMA; Mbunge wa Tanga Mjini, Kassim Mbaraka amehoji bungeni ni lini ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Bandari ya Tanga – Kilimanjaro – Arusha – Singida hadi Musoma yenye urefu wa kilometa 1108 utaanza.

Akijibu swali hilo bungeni leo Mei 19, 2026, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema serikali kupitia TRC imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya kuunganisha reli ya Bandari ya Tanga na mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Singida hadi Musoma.

“Kwa sasa, hatua inayoendelea ni kuhuisha (review) tafiti hizo ili kuendana na mahitaji ya sasa ikiwemo ushirikishwaji wa makampuni ya madini yanayowekeza kwenye ushoroba huo.

“Aidha, serikali inaendelea kufanya majadiliano na Kampuni mbalimbali ili kufanya uwekezaji wa reli hii ya kimkakati,” amesema Naibu Waziri.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button