UGANDA : SERIKALI ya Uganda na Kampuni ya Ujenzi ya Uturuki Yapi Merkezi zimetia saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme wenye urefu wa kilomita 272 (maili 169) ili kukuza biashara za kikanda.
Mratibu wa Mradi wa Reli ya Standard Gauge nchini Uganda, Perez Wamburu, amesema awamu ya kwanza itaanza kujenga njia ya reli ya umeme ya kilomita 1,700 itakayogharimu euro bilioni 2.7 sawa na dola Bilioni Tatu .
Ujenzi huo umepangwa kuanza Novemba mwaka huu utakaoweza kuongeza biashara na kupunguza gharama za usafiri.
Awamu ya kwanza ya ujenzi utaanzia katika mji mkuu wa Kampala hadi Malaba kwenye mpaka na Kenya, kuiunganisha Uganda na mitandao mingine ya reli ya jirani .