Ujenzi wa mfumo wakusaidia mtiririko mzuri wa utendaji kazi waanza

UJENZI wa mfumo wa kieletroniki wa utendaji kazi za mapitio, tathmini na utafiti wa sheria mbalimbali za Tanzania Bara umeanza.

Ujenzi huo utarahisisha utekelezaji wa majukumu, kupunguza gharama, na kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za nyaraka.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Griffin Mwakapeje ameeleza hayo alipofungua kikao cha wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( Tehama), kutoka Taasisi mbalimbali.

Advertisement

Mwakapeje amesema mfumo huo utakapokamilika utasaidia kurahisisha Mtiririko wa utendaji kazi, kufanya tathmini mbalimbali zitakazosaidia kubaini idadi ya mapendekezo ya Tume yaliyotumika katika maboresho.

Pia kuunda sheria mpya na utapunguza gharama wakati wa kuandika maandiko mbalimbali.

“Serikali imeridhia Uwepo wa mfumo huo na ni ukweli kwamba utawasaidia sana watafiti wetu katka utendaji kazi za Mapitio, Tathmini, na Utafiti wa Sheria mbalimbali,” amesema..

Amewataka wataalamu hao kuhakikisha mfumo unaweza kuwasiliana au kushirikiana na mifumo mingine ili dhana ya kurahisha utendaji kazi iweze kupatikana kwa urahisi.

Amesema kwa kutumia mfumo huo kutasaidia kupunguza gharama na muda kwa kuwa utakuwa na uwezo wa kuwasiliana na mifumo mingine ya Taasisi za Kisheria ikiwemo mifumo ya Wizara ya Katiba na Sheria, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na mifumo ya Mahakama.

Ameongeza Tanzania kuna sheria zaidi ya 450 ambazo zinapaswa kuzifanyia mapatio ili kuona zinaendana na uhalisia katika mazingira ya sasa.

 

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *