Ujenzi yaja na vipaumbele sita bajeti 2026/27

DODOMA; Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega leo Mei 20 2026, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa na vipaumbele sita.
Ametaja vipaumbele hivyo ni kuendelea na ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano hususan katika majiji na miji inayokua kwa kasi.
“Kuendelea na Ujenzi wa barabara zinazounganisha makao makuu ya mikoa, Tanzania na nchi jirani na maeneo ya kimkakati.

“Kuendelea na ukarabati na matengenezo makubwa ya maeneo yenye changamoto katika barabara kuu na za mikoa.
“Kuendelea na kuimarisha usafiri na miundombinu ya vivuko
“Kuendelea kuwajengea uwezo wataalam na wakandarasi wa ndani katika masuala ya ujenzi.
“Kuendelea na ujenzi wa majengo ya Serikali na nyumba za gharama nafuu,” amesema Waziri Ulega.



