UJERUMANI : Aliyewahi kuwa Rais Horst Köhler afariki dunia

UJERUMANI : ALIYEWAHI KUWA Rais wa Ujerumani Horst Köhler amefariki dunia  leo jumamosi (01.02.2025) baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Köhler aliyeiongoza Ujerumani kati ya mwaka 2004 hadi 2010, alifahamika kama muungaji mkono mkubwa wa bara la Afrika na amefariki akiwa na umri wa miaka 81.

Rais wa sasa wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema taifa lake limempoteza mtu muhimu aliyefanya mambo makubwa kwa nchi na dunia yote.

Advertisement

Kansela Olaf Scholz ametuma pia salamu za rambirambi kufuatia msiba huo na amemwelezea Rais huyo wa zamani wa Ujerumani kama “mwanasiasa  mwenye kujitolea aliyefanya kazi kwa ajili ya kuimarisha haki duniani.

Kabla ya kuwa Rais wa Ujerumani, Horst Köhler alikuwa Mkuu wa Shirika la Fedha duniani IMF pia alishika wadhifa wa Urais baada ya kupendekezwa na kiongozi wa upinzani wa wakati huo Angela Merkel ambaye baadaye alikuwa Kansela.

SOMA: Ujerumani yaitisha uchaguzi mpya

 

 

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *