UJERUMANI : SERIKALI ya Ujerumani imeingia katika mivutano ya kisiasa baada ya serikali yake ya muungano wa vyama vitatu kuvunjika.
Haya yamejiri kufuatia miezi kadhaa ya malumbano ya ndani kwa ndani kati ya vyama hivyo ambapo ikamlazimu Kansela Olaf Scholz kumuachisha kazi waziri wake wa fedha, Christian Lindner wa chama cha Free Democrats, FDP, jambo lililokipelekea chama hicho kujitoa katika muungano huo.
Chama cha Social Democrats, SPD, na kile cha wanamazingira cha Kijani ndivyo vilivyosalia katika serikali ya muungano iliyopoteza wingi wa viti bungeni. SOMA: Watu 8 wakamatwa Ujerumani kutaka kuipindua serikali