Watu 8 wakamatwa Ujerumani kutaka kuipindua serikali

UJERUMANI : JESHI la Polisi nchini Ujerumani limewakamata washtakiwa nane wa kundi la  wanamgambo wenye mitazamo tofauti na serikali wanaoamini ubaguzi wa rangi wanaotuhumiwa  kutaka kuipindua Serikali ya Ujerumani .

Katika taarifa iliyotolewa awali  na waendesha mashtaka imesema kuwa washtakiwa hao ni sehemu ya shirika lililoundwa Novemba mwaka 2020 wanaotaka kujitenga kutoka jimbo la Saxony.

Miongoni mwa washtakiwa hao, washtakiwa wanne ni waasisi wa kundi hilo na wengine walikamatwa katika miji ya mashariki mwa Ujerumani ya Leipzig, Dresden na Meissen.

Advertisement

SOMA : Ujerumani yatoa neno ushirikiano na Tanzania