Ujerumani kuwekeza Euro bilioni 4 nishati ya kijani Afrika

Olaf Scholz

UJERUMANI inapanga kuwekeza Euro bilioni 4 katika miradi ya nishati ya kijani barani Afrika hadi mwaka wa 2030, Kansela Olaf Scholz amesema.

Taifa hilo linahitaji kuagiza kiasi kikubwa cha hidrojeni ya kijani kutoka Afrika, ikiwa inataka kufikia lengo lake la kutotoa hewa sifuri ifikapo mwaka 2045, alisema katika kongamano la wafanyabiashara wa Ujerumani na Afrika mjini Berlin.

Jukwaa hilo lilitanguliwa na mkutano wa kilele wa “Mkataba wa G20 na Afrika” ambao unalenga kuibua uwekezaji barani Afrika kwa kuratibu ajenda za maendeleo za nchi zinazozingatia mageuzi na kubainisha fursa za biashara.

Advertisement

“Uzalishaji wa hidrojeni unahitaji uwekezaji mkubwa mwanzoni, kwa hivyo ishara wazi za ushirikiano wa muda mrefu na wa kudumu zinahitajika.” alisema Scholz.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *