Ukarabati Uwanja Ndege Mtwara safi

UKARABATI na upanuzi wa miundombinu ya kiwanja cha ndege mkoani Mtwara umefikia asilimia 96.

Maneja wa kiwanja hicho, Samuel Mruma amesema kuwa ukarabati kwa sasa upo hatua za mwisho kabisa za kumalizia kazi mbalimbali, ikiwemo usindikaji wa taa za kuongozea ndege, ili kuwezesha kufanya kazi saa 24, ambapo kwa sasa kiwanja hicho kinafanya kazi kwa saa 12 tu.

Amesema serikali ilitoa kiasi cha Sh bilioni 56.7 kwa ajili ya upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya kiwanja hicho, ili kukipa hadhi ya kimataifa.

Upanuzi huo ulihusisha upanuzi wa njia za kurukia na kutua ndege (runaways), ujenzi wa njia za maungio, eneo la maegesho ya ndege na uzio wa ndani.

Miundombinu mingine iliyojengwa ni barabara ya kiusalama ndani ya kiwanja, maegesho ya magari.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x