UKRAINE : SERIKALI ya Ukraine imethibisha kupokea miili ya wanajeshi 563 kutoka kwa mamlaka ya Urusi ambao wengi wao ni wanajeshi waliouawa katika mapigano katika eneo la mashariki la Donetsk.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa hii leo imesema kuwa miili mingine 320 ilirejeshwa kutoka eneo la Donetsk na mingine 89 ilirejeshwa kutoka Bakhmut katika mji uliotekwa na Urusi mwezi Mei mwaka jana na 154 ilirejeshwa kutoka vyumba vya kuhifadhia maiti nchini Urusi.
Tangu kuanza kwa vita kati ya Urusi na Ukraine hawajaweza kutoa idadi kamili ya wanajeshi waiouawa kwenye mapigano. SOMA: Putin yuko tayari kumaliza vita Ukraine