Ukraine yadai mapema kushiriki mkutano wa amani

WASHINGTON: RAIS wa Marekani, Donald Trump, alitangaza kwamba Ukraine itashirikishwa katika mazungumzo ya amani na Russia, licha ya kwamba Kyiv imeeleza kuwa ni mapema sana kuzungumza na Moscow katika mkutano wa usalama unaotarajiwa kufanyika leo Ijumaa.

Akizungumza na waandishi wa habari kutoka White House, Trump amesema kwamba Ukraine itakuwa na nafasi kwenye meza ya majadiliano yoyote ya amani na Urusi ili kumaliza vita.

“Ukraine inahusishwa kwenye mazungumzo. Tutakuwa na Ukraine, na tutakuwa na Urusi, na tutakuwa na watu wengine wengi watakaoshiriki,” Trump amesema.

Advertisement

Alipoulizwa iwapo anamuamini Rais Vladimir Putin, Trump alijibu, “Naamini kwamba atataka kuona hatua fulani ikifanyika. Namuamini kuhusu suala hilo.”

Trump alifafanua kuwa maafisa wa Marekani na Urusi wanatarajiwa kukutana leo Ijumaa huko Munich, na kwamba Ukraine imealikwa pia.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *