Ukraine yalaumiwa kutumia phosphorous katika mashambulizi

URUSI : WIZARA ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema Ukraine imekuwa ikitumia kemikali ya sumu aina ya Phosphorous katika mashambulizi yake ya droni, hasa yale yaliyofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Msemaji wa wizara hiyo, Maria Zakharova, alisisitiza kuwa Urusi ina ushahidi wa matumizi ya kemikali hiyo na kuihusisha na Ukraine.

Hata hivyo, hakukuwa na tamko rasmi kutoka kwa upande wa Ukraine, ingawa nchi hiyo pia imekuwa ikituhumu Urusi kwa kutumia kemikali hiyo.

Advertisement

Pia, Urusi imetangaza kwamba itachukua hatua za kujibu vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya, ambavyo Moscow inavyosema ni tishio kwa usalama wa nishati duniani. SOMA: Ukraine yakanusha kupeleka drone Mali