Ukraine yashambulia tena kiwanda Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

KIWANDA cha kusafisha mafuta kilicho katika Mkoa wa Krasnodar kusini mwa Urusi kimeshambuliwa na ndege zisizo na rubani za Ukraine siku ya Ijumaa asubuhi na kushika moto, maafisa wa dharura wamesema.

Chombo cha habari cha Baza kimechapisha video ya moshi mweusi ukitoka katika Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Ilsky. Kulingana na huduma za dharura, moto huo ulizimwa haraka, na hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Kituo hicho pia kilishambuliwa na ndege kadhaa zisizo na rubani mapema Alhamisi asubuhi, ambapo moto pia ulizuka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *