“Nyama ya mbuzi inaongeza maumivu magotini”

DAKTARI bingwa bobezi wa nyonga na magoti wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dk Antony Assey amesema ulaji wa nyama ya mbuzi unaongeza dalili kwa baadhi ya watu wenye ugonjwa wa maumivu ya magoti.

Akizungumza na HabariLEO mapema hii leo Dk Assey amesema hali hiyo inatokana na vinasaba vya nyama ya mbuzi kuwa moja wapo ambacho kinachochea kwa dalili hizo kwahiyo watu wanaoumwa matatizo hayo wanapata ushauri baada ya kufanyiwa uchunguzi.

SOMA: Watu tisa kupatiwa huduma mpya MOI

“Ulaji wa nyama ya mbuzi hauleti ugonjwa huo ila unaongeza dalili za ugonjwa huo kama mtu anatatizo anashauriwa kitu gani wanafanya na chakula gani wale na chakula kipi waache.

Dk Assey amesema takwimu zinaonesha watu wanapofika zaidi ya miaka 50 matatizo ya magoti yanaanza.

SOMA: MOI yawashika mkono wenye matatizo ya viungo

“Umri wa miaka 60 hadi 65 asilimia 50 watakuwa na aina fulani ya maumivu ya magoti na nyonga na umri unavyokwenda haja ya kufanyiwa upasuaji inajitokeza.

DK Assey amesema mgonjwa akifanyiwa upasuaji baada ya miaka 15 upasuaji unarudiwa kwaajili ya kubadilisha kifaa kwasababu kinachakaa.

Habari Zifananazo

Back to top button