ULAYA : MAWAZIRI wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uholanzi na Ubelgiji wanakutana mjini London kujadili tatizo la uhamiaji haramu.
Viongozi hao wanatarajia kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya makundi ya uhalifu yanayohusishwa na vitendo vya uhamiaji haramu barani Ulaya.
Miongoni mwa mambo muhimu watakayojadili katika kikao hiki ni kudhoofisha makundi ya magendo na kuhakikisha wanaojishughulisha na shughuli hizo wanafikishwa mahakamani.
Wawakilishi wa Tume ya Ulaya na shirika la kulinda mipaka ya Ulaya Frontex na lile la Polisi ya Ulaya Europol watashiriki pia mkutano huo ili kuelezea mpango kabambe wa utekelezaji wa hatua hizo kwa mwaka ujao wa 2025.
Tangu kuanza kwa mwaka huu, takriban wahamiaji 34,000 wamewasili Uingereza wakipitia baharini kwa kutumia mashua na karibu watu 70 wameripotiwa kufa maji. SOMA : Wahamiaji haramu 25 wapoteza maisha Comoro