Ulega ataka haki za wazawa miradi ya barabara

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameagiza mameneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wasimamie haki na maslahi ya wafanyakazi wazawa kwa wakandarasi kwenye miradi ya ujenzi barabara.
Aidha, serikali imeruhusu magari ya abiria na magari madogo yatumie kwa muda barabara ya mabasi yaendayo haraka (BRT) Awamu ya Tatu mkoani Dar es Salaam inayojumuisha Barabara ya Nyerere na Bibi Titi, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hadi Gongo la Mboto.
Ulega alitoa maagizo hayo Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za BRT na kuona uharibifu uliofanywa kwenye baadhi ya vituo vya mabasi hayo.
SOMA: Mikataba ya bil 507/- yasainiwa mwendokasi
Kuhusu barabara zinazojengwa na kampuni za ujenzi za kigeni nchini, Ulega aliagiza wakandarasi wahakikishe haki na maslahi ya wazawa yanazingatiwa kwa mujibu wa mikataba.
“Tunataka vijana hao waheshimiwe, utu wao ulindwe na haki zao wapewe ndani ya muda kwa mujibu wa mikataba yao, acheni kutengeneza visirani kwa vijana kuchukia viongozi wao kwa sababu ya nyie kutowajibika, changamoto zao zitatueni mko nao kwenye hii miradi, wajibikeni,” alisema Ulega.
Akiwa Buguruni kwenye ujenzi wa barabara ya BRT eneo la Bakhresa alisikiliza kero na changamoto za wafanyabiashara ya mbao ambao waliomba eneo la maegesho kwa ajili ya kushusha na kupakia mbao.
Ulega ameagiza wataalamu wanaosimamia ujenzi wa barabara hiyo waangalie uwezekano huo kitaalamu na wamshauri.
Akiwa Gongo la Mboto kwenye kituo cha BRT, kilichoharibiwa kwenye vurugu za Oktoba 29, mwaka huu, Ulega aliwataka vijana kutunza amani na kutokubali kushawishiwa kuiharibu.
Awali, akitoa taarifa kuhusu mradi wa BRT awamu ya tatu kuanzia katikati ya Dar es Salaam hadi Gongo la Mboto, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi ya Tanroads, Malima Kusesa alisema mkandarasi ni Sino Hydro kutoka China na anautekeleza kwa gharama ya Sh bilioni 232.6.
Alisema mradi unatekelezwa kwa miezi 42 na ulipaswa kukamilika Desemba mwaka huu na hadi sasa umefikia asilimia 96 ambayo ni zaidi ya mpango wa mkandarasi.
Kuhusu kuitumia barabara hiyo kwa muda, Ulega alisema, “Tumezungumza na mwenzangu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu maagizo ya Rais Samia Suluhu ya hizi barabara za mwendo kasi ambazo zimekamilika na bado huduma hazijaanza, turuhusu mabasi madogo ya abiria na watu binafsi kuzitumia kuwahi kwenye shughuli na kazini na kupunguza msongamano,” alisema Ulega.
Alisema kwa sasa utaratibu wa jinsi ya kuzitumia unaandaliwa na maelekezo yatatolewa.
Akiwa eneo la Barabara ya Sam Nujoma unakotekelezwa pia mradi wa BRT, Ulega alimpa mkandarasi miezi miwili kukamilisha kazi aliyopaswa iwe imekamilika hadi sasa.
Agizo hilo alilitoa pia kwa mkandarasi anayetekeleza ujenzi kama huo Barabara ya Bagamoyo kipande cha Mwenge hadi Tegeta na kusema amempa miezi miwili kukamilisha kazi vinginevyo serikali itaangalia jinsi ya kuvunja mkataba nae.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com