MJADALA katika toleo lililopita ulibainisha kuwa, maboresho ya kodi na miundo ya ujumuishaji ya hatua kwa hatua ni muhimu katika kutumia mapendekezo haya kwa vitendo halisi.
Ingawa kurahisisha mchakato wa usajili, kulipa kodi kwa awamu na kutumia nyenzo za kidijiti ni muhimu katika urasimisha wa sekta isiyo rasmi nchini, ufanisi wake unaweza tu kupimwa kupitia matokeo yanayoonekana.
Hatua inayofuata katika mjadala huu inakita nguvu kutoka muundo wa kisera hadi utekezaji halisi huku pia ukiangalia namna mataifa yenye muundo sawa wa kiuchumi yalivyofanikiwa kutoka kutokuwa rasmi hadi katika
ujumuishi.
Kwa kutumia mifano kutoka Tanzania na katika nchi nyingine, tunaweza kufanya tathmini za mafanikio yanayotokana na motisha/vivutio zilivyoratibiwa sawia, ufumbuzi wa kidijiti na mikakati wazi katika utekezaji kodi kwa hiari.
Kipengele hiki kinajikita katika mafanikio ya uchumi usio rasmi nchini Tanzania pamoja na uchanganuzi linganifu
kutoka mataifa mengine. Mifano hii itatumika kama mwongozo wa maboresho yanayotekelezeka ukisisitiza mambo muhimu ya kujifunza, changamoto na athari zinazopimika zinazoweza kuelezea juhudi zinazoendelea Tanzania.
Kwa kuunganisha nadharia na vitendo, mjadala huu unalenga kusisitiza kuwa maboresho ya kodi lazima yaitikie hali halisi ya wafanyabiashara wasio rasmi ili kuhakikisha kuwa, utekelezaji wa kanuni na sheria za kodi si tu jukumu la udhibiti, bali kuelekea ukuaji wa biashara, usalama wa kifedha na ustahimilivu wa uchumi wa taifa.
Imarisha ukusanyaji kodi
Mfanyabiashara wa Handeni, Tanga, Esther Kihiyo anasema maendeleo ya teknolojia ni nguzo muhimu katika mapinduzi ya ukusanyaji kodi nchini.
Anasema matumizi ya stempu za kodi za kidijiti yanaweza kuimarisha kwa kiasi kikubwa ulipaji kodi na kuhakikisha biashara zinazingatia na kutekeleza kwa urahisi kanuni za kodi.
Kwa mujibu wa Kihiyo, kuongeza muunganiko wa malipo kwa njia ya simu kupitia majukwaa kama M-Pesa, Mixx by Yas (zamani Tigo Pesa) na Airtel Money kutarahisishia wafanyabiashara wasio rasmi kufanya malipo madogo ya kodi na malipo ya kodi yanayoongezeka kuliko kukumbana na mzigo mkubwa kwa mara moja.
Kimsingi, kadiri uchumi wa kidijiti unavyopanuka, unazidi kuwa muhimu kuunda mfumo wa kodi kwa biashara za
kielektroniki zinazofanya kazi kupitia mitandao ya kijamii.
Ofisa Mwandamizi wa Kodi nchini Kenya, hivi alizungumzia athari za ufumbuzi wa masuala ya kodi kidijiti akisema,
“Ubunifu huu ulibadili mkakati wetu wa kukusanya kodi na kusababisha kuwapo kwa ongezeko la asilimia 33 ya utekelezaji wa sheria za kodi miongoni mwa biashara zisizo rasmi ndani ya miaka mitatu. Tanzania inaweza kupata mafanikio kama hayo kwa kuweka ufumbuzi huu kadiri ya hali yake ya soko.”
Mchambuzi kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) anasema endapo ufumbuzi wa kodi kidijiti utainua kiwango cha ulipaji kodi Tanzania kutoka asilimia 26 hadi ziada ya asilimia 33 ya ziada, utawezesha biashara mpya kati ya 600,000 hadi 700,000 zilizosajiliwa ndani ya miaka mitatu, mabadiliko yataongeza wigo wa vyanzo vya kodi kwa kiasi kikubwa na hivyo, kuimarisha hali ya utulivu wa kiuchumi.
Kwa kutumia ubunifu wa kodi kidijiti, Tanzania inaweza kurahisisha utekelezaji wa kodi, kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kufungua vyanzo muhimu vya mapato ambavyo havijatumika katika sekta isiyo rasmi. Utekelezaji wa mifumo rafiki ya kodi kwa watumiaji na mifumo ya kiteknolojia unaweza kuchochea ushiriki wa hiari na ukuaji endelevu wa uchumi.
Kukuza uaminifu
Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Victor Tesha, kurejesha na kudumisha hali ya kuaminiana baina ya mamlaka za kodi na wafanyabiashara wasio rasmi ni suala muhimu katika kukuza utamaduni wa wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari.
Anasema kampeni za wazi katika uhamasishaji wa umma zinazoonesha wazi namna mapato ya kodi yanavyowekwa katika huduma muhimu za umma ikiwamo miundombinu, huduma za afya pamoja na huduma za elimu
zitakavyosaidia kujenga upya mitazamo ya watu na kujenga matashi mema kwa wafanyabiashara wasio rasmi.
Kwa mujibu wa Tesha, ili kuziba pengo hilo lazima kuwe na uanzishwaji wa ofisi za kodi katika vituo visivyo rasmi vya biashara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata moja kwa moja msaada na taarifa sahihi na kwa wakati.
Anapendekeza kuwapo huduma za utatuzi wa mizozo na kuhakikisha haki za watu zinaheshimiwa.
Kanuni hizo zitashughulikia masuala yanayohusu kodi isiyo ya haki pamoja na kupunguza mivutano baina ya
mamlaka za kodi na wamiliki wa biashara. Kwa kutekeleza hatua hizi, ulipaji kodi utabadilika kutoka kuonekana ni mzigo mzito hadi kuwa ubia shirikishi unaonufaisha wafanyabiashara na uchumi kwa ujumla.
Mshauri wa Sera katika Wizara ya Fedha nchini aliyetaka jina lake lisitajwe gazetini, anasisitiza mtazamo huu akisema, “Wafanyabiashara wanaposhuhudia manufaa yanayoonekana wazi kutokana na kodi zao kwa shughuli za
maendeleo kama kuboresha miundombinu ikiwamo ya barabara na huduma za afya, wana uwezekano mkubwa wa
kulipa kodi bila shuruti.
“Lengo letu ni kupunguza ripoti zinazohusu unyanyasaji unaohusiana na masuala ya kodi kwa angalau asilimia 50
katika miaka miwili ijayo.”
Makadirio yaliyopo yanaonesha kuwa, mfanyabiashara mmoja kati ya wanne (asilimia 25) ananyanyaswa. Kwamba, kufikia punguzo la asilimia 50 kungepunguza idadi hii hadi takriban asilia 12-13, hivyo kuongeza imani katika mfumo wa kodi.
Kwa kutoa kipaumbele katika uwazi, upatikanaji pamoja na haki, Tanzania itapa mazingira ya kodi ya ushirika zaidi na hatimaye kuchochea biashara zisizo rasmi kuingia katika uchumi rasmi huku ikiimarisha mapato ya serikali na utulivu wa kiuchumi.
Urasimishaji kupitia vivutio vya kifedha
Ofisa wa Benki ya Dunia nchini Tanzania anasisitiza kuwa, maboresho ya udhibiti, motisha/vivutio vya kifedha
ni muhimu ili kuchochea urasimishaji wa biashara.
Miongoni mwa mikakati yenye athari kubwa ni kutoa mikopo ya riba nafuu kupitia programu zinazosaidiwa na
serikali zinazoweza kupunguza vikwazo vya mtaji na kuwawezesha wajasiriamali wadogo kuwekeza katika ukuaji wa biashara.
Ofisa mmoja wa ngazi za juu katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) anapendekeza kuwapo punguzo la kodi kwa uwekezaji wa biashara kama vile ununuzi wa vifaa au uboreshaji wa miundombinu kunakoweza kufanya urasimishaji kuvutia na kuwa chaguo muhimu kwa kampuni zisizo rasmi.
Mshauri wa masuala ya uchumi kutoka Mbeya, Julius Mwakalebela anasisitiza athari za vivutio vya kifedha akisema, “Kuwezesha upatikanaji wa makato ya mikopo na uwekezaji si tu kwamba huchochea ukuaji wa biashara, bali pia huunganisha zaidi mashirika yasiyo rasmi katika mfumo wa kifedha.”
Anasema nchi ya Ethiopia ni mfano bora, ambapo mpango wa huduma za kifedha zinazotolewa kwa wasioweza
kupata mikopo au huduma za kifedha katika taasisi kubwa za kifedha kama benki ulisababisha kuwapo ongezeko la asilimia 19 katika urasimishaji wa biashara katika kipindi cha miaka mitatu.
Kwa mujibu wa Mwakalebela, Tanzania ikitoa motisha sawa za kifedha itafikia ongezeko la asilimia 15 hadi 20 katika biashara zilizorasimishwa hivyo, kuwezesha kuwapo utulivu mkubwa na endelevu wa kiuchumi kwa muda mrefu
katika sekta ya biashara ndogo.
Aidha, Tanzania itaweka mazingira shirikishi zaidi ya kiuchumi na hivyo, kuziba pengo baina ya sekta isiyo rasmi na sekta rasmi huku pia ikikuza mapato ya taifa na kuimarisha ustahimilivu wa biashara.
Muundo wa kodi kwa sekta mahsusi
Kwa mujibu wa Mshauri wa Biashara ambaye pia ni Mtaalamu wa Kodi aliyeko Katavi, Fatma Kiwelu, kwa kuzingatia hali mbalimbali za sekta isiyo rasmi nchini, sera ya kodi ya aina moja kwa wote haiwezi kutumika na wala
haina ufanisi badala yake, mfumo wa kodi inayoongezeka ambapo viwango vya kodi huwekwa kadiri ya viwango
tofauti vya mapato na masharti maalumu ya sekta, utakuza usawa na kuchochea ulipaji kodi.
Anasema kwa biashara nyingi ndogo, kiwango cha wastani cha kodi cha asilimia 2 – 3 ya mapato kinawezekana zaidi kuliko tozo za juu zisizobadilika kwani zinaweza kukandamiza ukuaji na kuzuia utekelezaji wa kanuni na sheria za kodi.
Muundo ya kodi unaoakisi hali halisi ya utendaji katika sekta mahususi kama madereva wa bodaboda, baba/mamalishe na mafundi kunaweza kuchochea ufanyaji biashara endelevu huku ukichochea zaidi ulipaji kodi kwa hiari.
Mtaalamu wa Sera za Kodi kutoka Uganda, Baingana Chepyegon, anasisitiza maoni haya akisema, “Mfumo wa kodi
kwa sekta mahsusi, mfumo wa kodi unaoendelea huainisha majukumu kwa kuzingatia hali halisi ya biashara.”
“Sera zinapochangia changamoto mahususi za kisekta, viwango vya ulipaji kodi huwa bora zaidi. Makadirio yetu
yanaonesha kuwa, mtindo kama huo unaweza kuongeza ukusanyaji wa jumla wa kodi kwa asilimia 10-15 katika
kipindi cha miaka miwili ya kwanza ya utekelezaji.”
Chepyegon anaongeza: “Kwa kutumia muundo wa kodi unaojumuisha zaidi na unaoweza kubadilika, Tanzania inaweza kupanua wigo wa vyanzo vyake vya mapato huku ikitengeneza mazingira ambapo biashara ndogo hustawi na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa”.
Mifano
Nguvu ya maboresho ya kodi yaliyoundwa sawia inaoneshwa dhahiri na mifano halisi kutoka Auckland, New
Zealand.
Mhitimu wa hivi karibuni katika Shule ya Biashara ya Massey, Tobias Mshana anaelezea kuhusu, James Rangi ambaye ni mchuuzi wa mitaani maarufu, machinga ambaye maisha yake yamebadilika kwa kiasi kikubwa kutokana na sera rafiki za kodi.
Anasema kwa miaka mingi, James amekuwa akifanya kazi kwa njia isiyo rasmi huku akielemewa na taratibu ngumu
za usajili na kutokuwa na uhakika wa kiwango cha kodi. Alipata bahati iliyombadili wakati kituo cha majaribio cha
usajili wa kodi kilipoanzishwa jirani naye kurahisisha mchakato na kuunganisha chaguo la kulipa kodi kidjiti.
Katika kipindi cha ndani ya miaka mitatu ya kurasimisha biashara yake, James amepata mkopo wa riba nafuu uliofadhiliwa na serikali hali iliyomwezesha kupanua shughuli zake na kuwekeza vifaa vifaa vya majokofu.
Mshana anaamini ikiwepo mipango sahihi na mikakati ya utekelezaji, maboresho kama hayo yanaweza kufanyika kwa mafanikio makubwa nchini Tanzania huku yakichochea ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wafanyabiashara
wadogo.
Naye mwanauchumi
aishiye Mwanza, Robert Haule anatoa maoni yake kuhusu namna mikakati bunifu ya kodi kutoka nchi jirani inavyoweza kutumika kama kielelezo kwa Tanzania.
Anazungumzia mkakati wa ulipaji kodi kwa awamu nchini Rwanda ambapo msamaha wa kodi kwa kipindi cha miaka mitatu kwa biashara ndogo zipatazo chini ya kiwango kilichowekwa ulivyosababisha ongezeko la asilimia 28 katika usajili wa biashara ndogo kwa miaka miwili pekee.
Mbinu hii iliruhusu biashara kuwekeza tena mapato, ukaleta utulivu wa fedha zao na kuwafanya wajiandae kwa
ajili ya kutozwa kodi. Hii inaoneesha kuwa, mabadiliko katika utekelezaji kodi yanaweza kuchochea utekelezaji wa sheria za kodi.
Haule anagusia pia mapinduzi ya malipo ya kodi kidijiti nchini Kenya. Anasema, kwa kuwezesha biashara ndogo kulipa kodi kupitia mifumo kama M-Pesa, Kenya ilipata ongezeko la asilimia 33 ya utekelezaji wa sheria za kodi ndani ya miaka mitatu.
Ufumbuzi huu wa kidijiti umeondoa vikwazo vingi vinavyohusishwa na ulipaji kodi wa ana kwa ana (kwa mikono).
Huu ni mfano ambao watunga sera wanapenda kukabili hali ya soko la ndani.
Kwa upande wake, Juliana Ngorora kutoka Kigoma anaelezea namna mfumo wa kodi uliorahisishwa wa Ghana kwa biashara zisizo rasmi pamoja na programu zilizolengwa za mafunzo ya biashara, ulivyochochea ulipaji kodi kwa hiari kwa asilimia 22.
Nchini Ethiopia, urasimishaji unaosaidiwa na fedha ndogo umesabanisha ongezeko la usajili wa biashara kwa
asilimia 19 katika kipindi cha miaka mitatu na kuonesha kuwa, upatikanaji wa mikopo na motisha ya kodi unaweza
kubadili kwa ufanisi biashara zisizo rasmi katika uchumi rasmi.
Mifano hii kwa pamoja inaonesha mageuzi ya kisayansi ya kodi, ujumuishaji wa malipo kidijiti pamoja na motisha za
kimkakati za kfedha zinavyoweza kuimarisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa kodi na kuchochea ukuaji wa biashara ndogo.
Kwa kutumia uzoefu huu wa kimataifa, Tanzania inaweza kuunda sera zinazowezesha biashara ndogo, kupanua wigo
wa kodi na kukuza utulivu wa uchumi wa muda mrefu.
Hitimisho
Tunapohitimisha mjadala huu kuhusu mikakati ya maboresho ya kodi inayolenga kurasimisha sekta isiyo rasmi
nchini, maono ya wazi ya siku zijazo yanaibuka.
Safari kutoka shughuli zisizo rasmi hadi uchumi imara na shirikishi si tu kwamba inahusu marekebisho ya sera, bali inahusu pia kubadilisha maisha na kuunda fursa. Kwa matumizi ya ubunifu wa kidijiti kama vile malipo ya kodi kidijiti na kurahisisha taratibu za usajili, Tanzania inaweza kuibua uwezo ambao haujatumiwa.
Mifano zaidi ya mafanikio kutoka sehemu nyingine inaonesha kuwa, maboresho ya kisayansi, yanayoendeshwa na
teknolojia yanaweza kusukuma tekelezaji wa sheria za kodi na kuwezesha wafanyabiashara wadogo.
Mifano hii inadhihirisha kuwa, wakati motisha za kifedha na miundo ya kodi inaweza kufikiwa inapoundwa
kulingana na hali halisi ilivyo, pia huwa ni vichocheo vya ukuaji endelevu. Kuaminiana baina ya mamlaka za kodi na wafanyabiashara kupitia ushirikiano wa wazi na msaada wa ndani huimarisha zaidi mchakato wa kuleta mabadiliko.
Kupitia juhudi za ushirikiano, pamoja na kuunganisha mipango ya serikali na hali halisi ya msingi, Tanzania inaweza
kujenga mfumo wa kodi ambao si tu kwamba utakusanya mapato, bali pia utachochea upanuzi wa biashara, ushirikishwaji wa kifedha na maendeleo ya taifa.
Mambo hayo yanatoa mwongozo wa maboresho yanayotekelezeka
Wanasisitiza watunga sera, viongozi wa jamii na wavumbuzi kufanya kazi pamoja katika kubuni ufumbuzi unaozingatia changamoto na fursa za kipekee za sekta isiyo rasmi ya Tanzania.
Kadiri tunavyoendelea, ahadi ya uchumi jumuishi zaidi na wenye ustawi inabaki kuwa ushuhuda wa maboresho ya
kodi yaliyotayarishwa vyema. Katika kulifanya hili, Tanzania iko tayari kufafanua upya uhusiano kati ya utawala na
ujasiriamali.
Aidha, iko tayari kubadili utekelezaji wa sheria kutoka wajibu pekee, hadi safari ya pamoja kuelekea ustahimilivu
na ukuaji wa uchumi.