Ummy awasilisha ujumbe wa Rais Samia Ethiopia

DAR ES SALAAM; Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Julai 8, 2024 amewasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe maalum wa Rais Samia kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Ethiopia, Sahle-Work Zewde.

Waziri Ummy pamoja na wajumbe wake katika safari hiyo wamepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Afrika, Innocent Eugene Shiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button