AZERBAIJAN: MJUMBE wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia maswala ya mabadiliko ya tabia nchi, Wopke Hoekstra amesema umoja wa ulaya utaendelea kutoa fedha kwa nchi masikini katika kupambana na ongezeko la joto duniani.
Hoekstra, amesema kuwa nchi zote tajiri zinazochafua hewa zina wajibu wa kutoa mchango wao.
Umoja wa Ulaya ndiye mchangiaji mkubwa wa fedha za kusaidia nchi maskini kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini unataka mataifa makubwa kama China pia kuchangia.
Nchi zinazoshiriki mkutano wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi wa COP 29 mjini Baku Azerbaijan, umesema kuwa nchi hizi zinapaswa kuendelea kulinda na kuheshimu miongozo ya mikataba ya kupambana na athari za tabia nchi katika nchi maskini.