Upatikanaji Nishati Safi Tanzania Umeongezeka

UPATIKANAJI wa nishati safi ya kupikia nchini Tanzania umeongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi 23.2 mwaka 2025, ongezeko la zaidi ya mara tatu ndani ya miaka minne. Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi, amesema mafanikio haya yanaonyesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha wananchi wanapata nishati safi, salama na nafuu, ikichangia kulinda afya, mazingira na kukuza uchumi.

Amesema Tanzania imeendelea kupanua matumizi ya nishati safi kupitia utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Kwanza wa Afrika wa Nishati Safi ya Kupikia ambapo nchi ilihamasisha ahadi ya dola bilioni 2.2 kuendeleza sekta hiyo barani Afrika.

Waziri Ndejembi pia amebainisha kuwa  Mei 2024, Rais Samia Suluhu Hassan alizindua Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2024–2034 unaolenga kuratibu sera, mifumo ya kifedha na ushiriki wa sekta binafsi ili kuongeza upatikanaji wa nishati safi. SOMA: Sekta ya fedha yatakiwa kusukuma nishati safi ya kupikia

Kwa mwaka huu, Serikali inatarajia kusambaza majiko banifu 200,000 na mitungi 450,000 ya LPG kwa ruzuku, pamoja na kuanza majaribio ya kulipia vifaa vya kupikia kwa umeme kupitia bili za TANESCO. Aidha matumizi ya kuni na mkaa yamepigwa marufuku katika taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 ikiwa ni pamoja na shule na vituo vya afya.

Waziri Ndejembi amesisitiza kwamba nishati safi ya kupikia ni sekta yenye fursa za ajira katika uzalishaji, usambazaji na matengenezo ya vifaa, na Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau wa ndani na kimataifa kuhakikisha malengo ya upatikanaji wa nishati safi yanafikiwa kwa ufanisi na endelevu.

 

Habari Zifananazo

5 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

    1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

    2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  2. I started this as a simple side hustle, and last month I made a little over $6,137 just working a few hours a day from my phone. If you want to check out how it works, the website has all the details.
    Here—>> http://www.giftpay7.vip

  3. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button