SOMALILAND : KIONGOZI wa upinzani wa Jimbo la Somaliland, Abdirahman Cirro ameshinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha mtandaoni cha Garowe kimesema kiongozi huyo wa upinzani wa chama cha Waddani anaongoza kwa asilimia 64 ya kura dhidi ya rais aliyoko madarakani Muse Bihi Abdi ambaye amepata asilimia 35.
Somaliland ni jimbo lililokuwa na utawala wake baada ya kujitenga na Somalia tangu mwaka 1991.