LITHUANIA : CHAMA cha upinzani nchini Lithuania “Social Democrats” kimepiga kura ya maoni bungeni na kuongoza dhidi ya Chama tawala “Homeland Union Party” kwa kutokuwa na imani na serikali kufuatia ongezeko kubwa la gharama za maisha na usalama wa nchi hiyo .
Chama cha Social Democrats kiliongoza kwa viti 33 baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 64 ya kura ambazo zilipigwa na bunge hilo lenye jumla ya viti 141 huku Chama tawala cha Homeland Union Party kikipata viti 6.
Taifa hilo lenye wakazi milioni 2.9 lina mfumo tofauti wa upigaji kura ambapo nusu ya viti vya bunge huchaguliwa kupitia wingi wa kura na viti vingine vilivyobaki kupitia uchaguzi wa marudio.
Iwapo chama cha Social Democrats kitafaulu kuunda serikali basi kinatarajiwa kuendeleza msimamo wa Lithuania dhidi ya Russia, pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya matumizi ya ulinzi wa nchi hiyo.
SOMA: Moldova kujiunga EU bado kitendawili