Upungufu wa maji wamuibua Malima Morogoro

MOROGORO: MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), na Bonde la Wami Ruvu kushirikiana na viongozi wengine wa serikali ya mkoa huo kusimamia udhibiti wa uchepushaji maji ili kuepusha kuendelea kwa upungufu wa maji.
Malima ametoa agizo hilo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati inayochukukiwa ya kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji ya uhakika katika Manispaa ya Morogoro.
Amesema amekuwa akipokea malalamiko ya ukosefu wa maji kutoka kwa wananchi wa manispaa hiyo na kuchukua hatua kuagiza wataalamu wa Moruwasa kupitia changamoto zote na kuwasilisha majibu ya changamoto hizo kwake.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo pia ameagiza mamlaka hiyo kuandaa ratiba ya mgao wa maji itakayowekwa wazi kwa wananchi ili kuifahamu.
“Kitengo cha mawasiliano cha MORUWASA kitoe namba ya simu itakayosaidia wananchi kutoa taarifa ya masuala ya maji pale watakapoyakosa siku ya mgao wao,”ameagiza Malima.
Pia amewasihia wanachi kutumia maji kwa ufanisi na kuacha tabia ya kuchepusha maji ya mito kwa ajili yaa kilimo cha umwagiliaji kwani kwa kufanya hivyo kusababisha wananchi wengine kukosa maji.
“Ni muhimu kwa wananchi kupewa uelewa wa kina juu ya wajibu wao katika kulinda rasilimali hizo ili kuzuia athari zaidi zinazoweza kusababisha upungufu wa maji,” amesema Malima.
Malima pia amewataka wananchi kutoharibu mazingira kwenye vyanzo vya maji huku akisisitiza kwa kipindi hiki cha upungufu wa maji , wananchi wanapaswa kujitahidi kuwa na vyombo vya kutosha vya kuhifadhia maji siku ya mgawo wao wa maji yatakapotoka
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, CPA Sais Kyejo, amesema upungufu wa maji unachangiwa pia na ubovu wa miundombinu ya maji hususan mabomba yanayomwaga maji hivyo kufanya upotevu wa maji yanayozalishwa kufikia asilimia 15 kwa siku kutokufikia wanachi.
Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA amesema wataalam wa Mamlaka hiyo wamefanya tathmini katika maeneo mbalimbali ya vyanzo vya maji na kubaini hali ya vyanzo hivyo si nzuri.
Kyejo amesema kujitokeza kwa hali hiyo ,kunachangia kupungua kwa wingi wa maji katika vyanzo hivyo na kusababisha huduma ya maji kutopatikana kwa kiwango kinachotakiwa.
Amesema Serikali inajitahidi kuboresha miradi ya maji iliyopo ukiwemowa Bwawa la Mindu ambao kwa sasa umefikia asilimia 44 hadi kukamilika kwake ambao utaongeza kiwango cha upatikanaji wa maji
Kyejo amesema asilimia kubwa ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wanapata maji kutoka Bwawa la Mindu ingawa upatikanaji wake umeathiriwa na shughuli za kibinadamu zinazofanywa kwenye vyanzo vya maji kama kilimo na ukataji miti.




Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com