URUSI: Mazungumzo ya silaha za nyuklia na Marekani hayaridhishi

URUSI: NAIBU WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Ryabkov, anayehusika na mahusiano na Marekani pamoja na udhibiti wa silaha, amesema kuwa hali ya mazungumzo kuhusu utulivu wa kimkakati wa nyuklia kati ya Urusi na Marekani bado hauridhishi.
Ryabkov alitoa maoni hayo mwezi uliopita baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kusema kuwa anapanga kupunguza matumizi ya silaha za nyuklia huku Ikulu ya Kremlin ilisema kuwa serikali ya Urusi inataka kuanzisha tena mazungumzo ya kupunguza silaha za nyuklia haraka iwezekanavyo.
SOMA: Ulaya wahofia matumizi ya nyuklia
Hata hivyo, Ryabkov alisema kuwa Marekani inataka kuhusisha China katika mazungumzo ya pande tatu, wakati Urusi ikipendelea mazungumzo ya pande tano.
Urusi imesema inataka pia Uingereza na Ufaransa kushirikishwa katika mazungumzo yoyote mapya kuhusu udhibiti wa silaha za nyuklia.



