BARAZA la juu la bunge la Urusi, limeidhinisha mikataba ya muungano na Jamhuri za Watu wa Donetsk na Lugansk na Mikoa ya Kherson na Zaporozhye.
Mikataba hiyo ilitiwa saini na Rais wa Urusi Vladimir Putin na wakuu wa mikoa minne ya zamani ya Ukraine Ijumaa wiki iliyopita. Mikataba hiyo ilithibitishwa kuwa halali na Mahakama ya Kikatiba mwishoni mwa juma na kupitishwa na Duma, Bunge la chini la Urusi.
Hatua ya hiyo ni sehemu ya mchakato wa kuyakubali maeneo hayo manne kama sehemu mpya za Urusi iliidhinishwa kwa kura ya kauli moja. Katiba ya Urusi itahitaji kurekebishwa ili uandikishaji huo ukamilike.