MAREKANI : URUSI yapinga azimio la Umoja wa Mataifa lililopendekeza usitishaji wa vita mara moja nchini Sudan kati ya jeshi la nchi hiyo na vikosi vya wanamgambo.
Azimio hilo ni pamoja na kuchukua hatua ya kuanza kupeleka msaada wa kibinadamu kwa mamilioni ya watu wanaohitaji.
China ni miongoni mwa washirika wa Urusi pamoja na mataifa waliunga mkono azimio hilo lililowasilishwa na Uingereza pamoja na Sierra Leone.
Waziri wa mambo ya nje nchini Uingereza David Lammy ameliambia baraza hilo hatua ya Urusi kuzuia azimio hilo ni fedheha hasa ukizingatia nchi hiyo inahitaji kurejesha amani yake.
Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitahadharisha kuwa Sudan imeshafika ukingoni kutumbukia katika baa la njaa.