MAREKANI : KITUO cha Maendeleo ya Kimataifa kilichoko Washington, CGD, kimeonya kuwa kusitishwa kwa misaada ya kigeni kutoka Marekani kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa nchi zinazoendelea.
Taarifa iliyotolewa na kituo hicho,inasema kuwa kusitisha misaada ya Marekani kwa mwaka mzima kunaweza kusababisha hasara ya zaidi ya asilimia moja ya pato la taifa kwa nchi 20 duniani.
Hatua hii inatokea chini ya wiki moja baada ya Rais Donald Trump kurejea Ikulu ya Marekani, ambapo shirika la USAID limewaambia mashirika yasiyo ya kiserikali kuwa watalazimika kusitisha shughuli zao mara moja kutokana na utawala mpya kusimamisha bajeti zake.
Pia, mkaguzi mkuu wa shirika la USAID, Paul Martin, ameondolewa kutoka nafasi yake, jambo linaloonyesha mabadiliko ya kimenejimenti katika shirika hilo.
Hii ni changamoto kubwa kwa nchi zinazotegemea misaada ya kigeni kutoka Marekani kwa ajili ya miradi ya maendeleo, afya, na elimu. SOMA: Musk: USAID ni shirika la kihalifu