Usajili wa wawekezaji TIC waongezeka asilimia 44

KITUO Cha Uwekezaji Nchini (TIC) kimesema mwamko wa usajili wa miradi ya wawekezaji umeongezeka kutoka wawekezaji 500 kwa mwaka 2023 hadi wawekezaji 901 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 44.5.

Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dr Binileth Mahenge amesema hayo baada ya kutembelea mradi wa uwekezaji wa kampuni ya wachimbaji ya Mwamba Mining katika kata ya Lwamugasa wilayani Geita mkoani hapa.

Mahenge amesema miradi 500 ya uwekezaji iliyosajiliwa mwaka 2023 ina thamani ya dola za kimarekani bilioni tano huku miradi 901 iliyosajiliwa mwaka 2024ina thamani ya dola za kimarekani bilioni 9.3.

Amesema mafanikio hayo yametokana na uboreshaji wa mazingira bora ya uwekezaji pamoja na na mabadiliko ya uwekezaji mwaka 2022 ambayo imeondoa vikwazo vingi kwenye usajili wa uwekezaji.

“TIC sasa hivi tuna kituo cha One Stop Center ambapo ukifika pale unaweza ukasajili na ukaanza shughuli zako ndani ya siku tatu”, amesema Mahenge.

“Tunaendelea kuhamasisha watanzania waje TIC kusajili na kuwekeza kwani kuna faida wazawa wanapata ikiwa ni pamoja na kuondolewa baadhi ya vikwazo.

“Hapa Geita mwaka jana walisajili miradi 18 na malengo ya mwaka huu ni kuweza kusajili miradi 50 kwa sababu mazingira ni rafiki, amesema Dr Mahenge.

Rais wa Kampuni ya Mwamba Mining, Eduard Cornew ameeleza kuguswa na sera rafiki katika sekta ya madini hususani kwa wazawa na wabia wanaokuja kuwekeza na kuahidi kupanua uwigo wa uwekezaji.

Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Kampuni ya Mwamba Mining, Thomas Cornew kutoka nchini Marekenai amrkiri kuwa tangu wamefika Tanzania wamepata ushirikiano mkubwa na hawajapata kikwazo kuwekeza.

Meneja wa Kampuni ya Mwamba Mining, Calvin Habil amesema mradi huo una thamani ya bilioni 8.5 umetumia miezi sita tangu kuanza hadi kufikia hatua ya majaribio kutokana na mazingira mazuri ya TIC.

“Ujenzi wa Mradi ulianza mwezi Mei, 2024 mapaka sasa tupo kwenye kipindi cha majaribio, kuweza kuona ufanisi wa kazi yetu tuna mpango wa kutanua plant yetu tuweze kuprocess tani 500 kwa siku”, amesema Calvin.

Mwakilishi wa Katibu Tawala mkoa wa Geita, Charles Chacha amesema mkoa una wawekezaji 16 wa kati sekta ya madini ambapo aliwaomba kuzingatia sheria kuanzia uchimbaji, uchejuaji na uchimbaji.

Ofisa Tarafa wa kata ya Busanda, Fred Muhagama amesema kwa kushirikiana na viongozi wa vitongoji, vijiji na kata wanasimamia kuhakikisha uwekezaji unafanyika bila kuathiri haki ya wananchi wa kawaida.

Habari Zifananazo

Back to top button