‘Ushahidi ambao haujawasilishwa hautofanyiwa kazi’

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande, amesema kazi za tume zinaongozwa na ushahidi uliowasilishwa ambao katika siku za mwisho kabla ya kuongezewa muda wa ziada, Watanzania zaidi wamekuwa wakiutoa hivyo kuamua kuchukua.

Akizungumza Dar es Slaam, Jaji Chande, alisema watu ambao wana ushahidi, lakini hawauwasilishi hautafanyiwa kazi, kwa kuwa tume inafanyia kazi ushahidi uliowasilishwa mbele yake.

“Kazi ya Tume inaongozwa na ushahidi. Mtiririko wa ushahidi ni mkubwa. Ndiyo maana tumeomba muda hatuwezi kuacha ushahidi uliotufikia.

Tunaamini muda tulioomba utatosha. Wengine wenye ushahidi tunawakaribisha. Sisi hatulazimishi watu kwa amri bali hiari katika kutoa ushahidi,”alifafanua Jaji Chande

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button