Ushindi Tuzo za Afrika uwe chachu kukuza sekta ya utalii

MWISHONI mwa wiki, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Tuzo za 32 za Utalii duniani 2025 maarufu World Travels Awards Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi.

Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa tuzo hizo kufanyika nchini tangu zilipoanzishwa mwaka 1993. Habari njema kwa Tanzania ni kwamba imeshinda tuzo 27 kati ya 60 zilizotolewa katika vipengele mbalimbali.

Na katika tuzo hizo, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) liliandika historia kwa kushinda tuzo saba, hatua inayoakisi dhamira na juhudi zake katika kulinda, kuhifadhi na kukuza utalii wa ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa tuzo hizo ni Hifadhi ya Taifa Serengeti ambayo kwa mara ya saba mfululizo ilitangazwa kuwa Hifadhi Bora Afrika, Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro imeshinda Tuzo ya Hifadhi Bora ya Milima Afrika, na Hifadhi ya Taifa Nyerere ilishinda kipengele cha Hifadhi Bora kwa Mandhari ya Kuvutia Afrika.

Aidha, Hifadhi ya Taifa Tarangire imeshinda Tuzo ya Hifadhi Bora kwa Utalii wa Tembo, Serengeti ilishinda Tuzo ya Hifadhi inayoongoza kwa kivutio cha wanyama wakubwa watano, Hifadhi ya Taifa Ruaha ilishinda Hifadhi Bora kwa Utalii wa Kitamaduni Afrika, na Kitulo ilitajwa kuwa Hifadhi Bora kwa Fungate Afrika.

Serikali imenyakua tuzo 11 zikiwamo za vivutio bora vya utalii, Bodi bora ya utalii Afrika, Nchi bora ya Utalii wa Safari Afrika na Uwanja wa Ndege bora Afrika, huku sekta binafsi ikitwaa tuzo 16 kwenye kampuni za kitalii, hoteli na huduma za kitalii.

Ushindi wa tuzo hizo katika tuzo hizi maarufu duniani ni kielelezo cha jinsi serikali na sekta binafsi zilivyofanya kazi kubwa katika sekta ya utalii nchini kiasi cha kutambulika kimataifa na kutuzwa kwa kazi hiyo kubwa na nzuri.

Ushindi kupitia tuzo hizi unathibitisha kuwa kazi nzuri inapaswa kuendelezwa hasa ikitiliwa maanani kuwa sekta ya utalii ambayo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeipa msukumo mkubwa.

Rais Samia mwenyewe amekuwa kinara katika kuimarisha sekta ya utalii akishiriki mara mbili katika filamu zenye kuitangaza Tanzania na vivutio vyake, jambo ambalo linapaswa kuendelezwa na kila Mtanzania katika nafasi yake.

Sisi tunaamini tuzo hizi ni kichocheo cha kuongeza nguvu na juhudi katika sekta ya utalii ili izidi kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi, kwa kuongeza mapato na pia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Tanzania.

Kwa msingi huo, tunaipongeza serikali na sekta binafsi kwa mafanikio haya makubwa, chini ya uongozi wa Rais
Samia na Wizara ya Maliasili na Utalii, wataimarisha mikakati ya kuimarisha sekta ya utalii, wataendelea kufanya
mambo makubwa zaidi ili si tu kushinda tuzo hizi mwakani bali pia kuifanya sekta iwe kinara katika kila kitu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Google pay 145$ dependably my last pay check was $8500 working 10 hours out of reliably on the web. My undeniably young family mate has been averaging 16k all through ceaseless months and he works around 24 hours dependably. I can’t trust in howdirect it was once I endeavored it out.This is my basic concern…HERE……… ­­W­­w­­w­­.­­J­­o­­i­­n­­S­­a­­l­­a­­r­­y.­­­C­­­o­­­m­­­

  2. I get paid over $130 1 to 3 hours working from home with 2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over $27k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless.
    Heress———–> http://www.now.jobs67.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button