Ushirikiano kipaumbele uongozi mpya ALAT

ARUSHA: Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Sospeter Mtwale amewataka viongozi wapya waliochaguliwa katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanafikiwa.

Mtwale ameyasema hayo jijini Arusha baada ya kutangazwa kwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, watakaodumu kwa muda wa miaka mitano.

Mtwale amesema ushindi wa viongozi hao ni dhahili kuwa wajumbe wana imani nao hivyo wakatekeleze majukumu yaliyo mbele yao kwa ufanisi na uadilifu.

Katika uchaguzi huo, Meya wa jiji la Mwanza, Sima Constantine Sima, ameiibuka mshindi kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa ALAT taifa baada ya kupata kura 273 kati ya kura 339 zilizopigwa.

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 45, huku Seif Daud akishika nafasi ya tatu kwa kura 17 kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Agneta Mpangile alibuka mshindi baada ya kupata kura 189 kati ya kura 337 zilizopigwa.

Akifuatiwa na Ali Mkaingwa aliyepata kura 118, na Solomon mabati aliyepata kura 29.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button