DODOMA : NAIBU Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis amesisitiza kuwa mapenzi ya jinsia moja hayaruhusiwi nchini Tanzania.
Akijibu swali bungeni mjini Dodoma,Naibu Waziri Mwanaidi amesema Tanzania ni miongoni mwa baadhi ya nchi barani Afrika zinazoendelea kulinda na kutetea tamaduni zake ili kulinda tamaduni na ustawi wa watu wake.
“haturuhusu mapenzi ya jinsia moja yawe faragha au hadharani tamaduni hizi sio za kwetu kama Tanzania,”amesema Naibu Waziri,
Aliongezea,“tutaendelea kutoa elimu kama serikali kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia na mapenzi ya jinsia moja ili kuhakikisha mila na desturi zinaimarishwa” Alimalizia.
Kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 154 ya sheria ya kanuni za adhabu sura namba 16 ya sheria ya Tanzania kinatamka bayana kuwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja au uhusiano wa kinyume na maumbile iwe faragha au hadharani ni kinyume cha sheria.