Utafiti ugonjwa zao la ndizi wafikia pazuri
UTAFITI wa kukabiliana na ugonjwa wa ndizi aina ya mshale unaojulikana kama mnyauko wa fuzari uko katika hatua nzuri.
Mtafiti mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ( TARI), Dk Mpoki Shemwela amesema hayo alipozungumza na HabariLeo katika maonesho ya mazao mbalimbali kuelekea kongamano la chakula mkoani Dar es Salaam lililoanza leo.
Dk Mpoki amesema utafiti huo umefikia katika hatua nzuri kwa kuwa mpaka sasa tayari aina mpya ya mshale imeshapatikana ipo katika majaribio ya awali katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Mbeya.
” Zaidi ya asilimia 90 ya aina hii ya mshale iliyofanyiwa utafiti inafanana na mshale asilia ambao unapendwa na wachaga.
” Una uzaaji wa kutosha, majaribio ya awali pamoja na wakulima waliozionja walizipenda, zina ladha inayofanana na mshale,” amesema.
Amesema kutokana na kupotea kwa zao hilo kwa utafiti unaoendelea unatoa matumaini mapya kwa wana Kilimanjaro.
Naye Mkuu wa Idara ya Uchechemuzi na Uratibu wa Rasilimali kutoka Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Kilimo ( IITA), Dk Regina Kapinga amesema maonesho ya utafiti wa mazao mbalimbali yaliyofanyika katika kituo Chao ni mojawapoi ya maandalizi ya kongamano kubwa la chakula nchini Tanzania.
Amesema kwenye maonesho hayo watu mbalimbali wamejionea tafiti za mazao mbalimbali ambazo zimefanyika kuanzia mashambani hadi kwenye uchakataji.