NIGERIA; Tajiri mkubwa Afrika Aliko Dangote, amewashangaza watu wengi wa Nigeria baada ya kusema hana nyumba nje ya nchi hiyo.
Dangote alisema anamiliki nyumba mbili nchini Nigeria ikiwemo nyumba moja ambayo iko katika mji wa Kano ambako alikozaliwa na nyingine iko katika mji wa Lagos.
Pia amesema akiwa katika ziara zake za kikazi katika mji mingine ndani ama nje ya nchi kwa kawaida anakodisha.
Katika jarida la Forbes la mwezi Januari lilimuandika Dangote kama mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mwaka wa 13 mfululizo licha ya kuwepo kwa matatizo ya uchumi nchini Nigeria.
Soma: Dangote kuzindua kiwanda cha kusafisha mafuta leo
Utajiri wake uliweza kupanda kwa dola za kimarekani milioni 400 zaidi mwaka jana, na kumpa jumla ya thamani ya dola za Marekani Bilioni 13.9.
Kwa sasa mfanyabiashara huyo ana umri wa miaka 66, ambaye amejitajirisha kwa kuuza saruji na sukari na mwaka jana alifungua kiwanda cha kusafisha mafuta katika kitovu cha uchumi cha Nigeria, Lagos.
Hatahivyo kauli ayke hii iliwashangaza watu wengi nchini humo, ambapo matajiri wengi wana sifa ya maisha ya kifahari na wengi wakimiliki nyumba mjini London, Dubai au hata Atlanta.
Matamshi yake yamezua hisia nyingi kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakisema ni uamuzi wa busara wa kibiashara kwani ni nafuu kulipa kodi kuliko kununua nyumba.
Dangote alisema sababu ya uamuzi wake ni kwamba anataka kuona Nigeria inakua.
“Sababu ya kutokuwa na nyumba London au Marekani ni kuwa nilitaka kuangazia ukuaji wa viwanda nchini Nigeria,” alisema.
“Nina shauku kubwa juu ya ndoto ya Nigeria na kando na nyumba yangu ya Lagos, nina nyumba nyingine katika jimbo langu la Kano, na nyingine ya kukodi huko Abuja.
“Ikiwa nitakuwa na nyumba kote Marekani na sehemu zingine, nisingeweza kutuliza akili na kufanya kitu kwa ajili ya watu wangu.”alisisitiza tajiri Dangote.
Dangote anadaiwa kumiliki makazi ya kifahari katika Kisiwa cha Banana maarufu cha Lagos, ambako Wanigeria wengi wenye hadhi ya juu pia wana majumba ya kifahari.
View this post on Instagram
Mchambuzi wa masuala ya umma, Sani Bala, alisema Dangote alikuwa akionesha mfano mzuri sana.
“Wanaijeria wanahitaji kuelekezwa upya kuelewa kumiliki majumba kadhaa sio mafanikio wakati pesa zingehitajika mahali pengine.
“Dangote alisema aliuza nyumba yake huko London mnamo mwaka 1996 na nina uhakika pesa zilizopatikana kutokana na mauzo zilirejeshwa katika biashara yake – huo ndio mfano wa kuiga,” amesema.
Chanzo: BBC