Utalii matibabu, wagonjwa Sierra Leone kutibiwa JKCI

DAR ES SALAAM: Wagonjwa wa Moyo kutoka nchi ya Sierra Leone watakuja kutibiwa hapa nchini hii ikiwa ni matunda ya utangazaji wa tiba utalii nchini.

Akizungumza wakati wageni kutoka nchi hiyo walipowasili katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Richard Kisenge amesema baada ya ugeni huo ambao umeambatana na mganga mkuu wa serikali wa nchi hivyo wameweza kuona mengi na kujifunza.

“Tumepata ugeni wa wenzetu kutoka Sierra Leone wamekuja kuona maendeleo haya kuanzia tulipoanza hadi sasa wamekuja kujifunza viongozi wetu wanavyotuongoza na kuwa na taasisi kama hii vilevile utendaji kazi wa wahudumu wetu wa afya wanavyofanya kazi ili wanapokwenda kuanzisha taasisi kwao wawe na uelewa wa kutosha.

Isome pia https://habarileo.co.tz/tanzania-yangara-utalii-wa-tiba-eac/

Ameongeza “Pili wamekuja kujifunza ili kuleta wagonjwa kutoka Sierra Leone kuja kutibiwa hapa kwani wamejionea wenye kuwa watatibiwa vizuri na hii ni sehemu ya tiba utalii ambayo rais pia ameifanya.

Amesema kuwa wamejifunza mfumo unatumika wa kupata dawa kutoka bohari ya dawa na uwekezaji wa vifaa tiba uliofanyika.

Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dk. Sartie Mohamed Kenneh amesema wamekuja kujifunza na kuangalia mifumo ya afya hali itakayoasaidia uboreshaji wa huduma katika nchi yao.

“Tunachangamoto ndio maana tuko hapa na tumeona Tanzania ni sehemu ya kujifunza hata kama sio kwa asilimia 100 lakini kuna vingi tumeona na tumelinganisha na sisi na tumeona tumejifunza.

Isome pia https://habarileo.co.tz/tanzania-kimbilio-matibabu-ya-kibingwa-kitaifa-kimataifa/

Amesema kutokana na ongezeko la magonjwa ya moyo ni muda sasa wa Wizara za Afya Afrika kufanya kazi kwa pamoja.

“Tutajaribu kuungana na kushirikiana iliwemo mafunzo na Tanzania ni bora tutumie rasilimali zetu Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi tiba shirikishi Dk Delila Kimambo ameeleza kuwa wanafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha huduma za moyo zinasambaa nchini.

“Hili sio la daktari tu kuna watu wengi wakiwemo mainjinia wa vifaa tiba vya moyo tunahakikisha usalama wa mgonjwa unafanyika kwa kiasi kikubwa kwani wagonjwa wanakuwa na mambo mengi sio moyo tu hivyo lazima kuwe na mtu anahakilisha usalama wa dawa zinapoingia kwa pamoja kwenye mwili wa mtu ,”amesisitiza.

Habari Zifananazo

Back to top button