Utangazaji redio kidijiti kuanza mikoa mitano

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema huduma za maudhui ya redio kidijiti (DSB) Tanzania zitaanza mikoa mitano.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabiri Bakari amesema kila mtoa huduma za urushaji maudhui hayo amepangiwa eneo moja la huduma katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mwanza na Mbeya. “Watoa huduma hao wameshinda zabuni iliyotangazwa na TCRA mwaka jana kwa urushaji kutumia bendi mbili za kimataifa za radio kidijiti,” alisema Dk Bakari.

Ameongeza : “TCRA imeainisha masafa ya wigo wa bendi ya megahezi (Mhz) 174 hadi 300 na kilohezi (KHZ) 525 hadi 1605 kwa ajili ya utoaji huduma za maudhui ya redio katika kila eneo la huduma”. Dk Bakari amesema TCRA imepanga mtoa huduma mmoja atapewa leseni kwa kila eneo la huduma kwenye mikoa hiyo ili kuongeza ufanisi katika matumizi ya masafa. SOMA: TCRA yahimiza umakini kulinda amani, umoja

Amesema utangazaji wa DSB Tanzania utaiwezesha nchi kukabili changamoto ya masafa adimu ya utangazaji wa redio, hasa kwa huduma za maeneo ya mijini na pia utawezesha kufikisha maudhui ya redio kwa hadhira pana zaidi. Dk Bakari amesema hadi kufikia Desemba mwaka jana masafa ya FM yalienea asilimia 59 ya eneo la Tanzania na yalifikia asilimia 84 ya watu.

“Teknolojia za DSB zinakuja kwa wakati muafaka kukabili msongamano huo wa masafa. Zinatumia masafa kwa ufanisi, zinahakikisha ubora wa sauti kwa wasikilizaji popote watakapokuwa,” alisema. Dk Bakari alisema DSB itafungua fursa za kusisimua kwa vituo vipya vya redio na huduma zitaenea zaidi na kufikia kila pembe ya Tanzania.

“Kwa kuanzisha huduma za utangazaji kwa teknolojia za DSB, Tanzania inaweka rekodi nyingine kwa kuwa ya kwanza kuendana na mabadiliko ya teknolojia za utangazaji za kidijiti kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini,” alisema.

Tanzania ilikuwa ya kwanza kwenye ukanda huu kuanzisha utangazaji wa televisheni mfumo wa ardhini kidijiti. Ilizima mitambo ya analojia Desemba 2014, miezi sita kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa na Shirika la Mawasiliano Ulimwenguni (ITU).

Habari Zifananazo

One Comment

  1. These mushroom edibles gummies were a pleasant surprise. The flavor was haler than expected, which already made them effort out from a luck of functional-style gummies on the market. The packaging looked clean, and the serving instructions were light to follow, which made the commodity feel more polished overall. They fit by nature into a daytime pattern and felt serviceable to keep on hand when something plain and straightforward was needed. Meticulous weave, solicitous taste, and an blanket outcome that feels sufficiently made.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button