UTEUZI: Ndumbaro, Bashungwa wahamishwa wizara

DAR ES SALAAM :Rais Samia Suluh Hassan amemteuwa Damas Ndumbaro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria awali alikuwa Waziri wa Utamaduni Sanaaa na Michezo.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Moses Kusiluka.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia Suluh Hassan amemteuwa Inocent Bashungwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kutoka Wizara ya Ujenzi.



