Utulivu watakiwa kesi mgawanyo rasilimali Chadema

DAR ES SALAAM: Jopo la mawakili wa Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Said Issa Mohamed, limewaomba wanachama wa chama hicho kuwa watulivu wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama katika kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa mali na rasilimali za chama.

Kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 inahusu mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali za chama kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Shauri hilo limefunguliwa na Mohamed kwa kushirikiana na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wakili waandamizi Gido Semfukwe akisaidiana na Shabaan Marijani na Alvan Fidelis, amesema kumekuwepo na dhana kwamba kesi hiyo imeletwa na kikundi cha watu wachache, jambo alilodai si sahihi.

“Ukweli ni kwamba katika shauri hili wapo viongozi waandamizi wa chama pamoja na wafuasi wengi wenye nia ya kuona chama kinakuwa mikononi mwa wanachama walio hadi ngazi za chini kabisa, si kumilikiwa na kikundi cha watu wachache,” amesema Semfukwe.

Amefafanua kuwa lengo la mashauri hayo ni kuleta uwiano sawia wa mgawanyo wa mali na ushiriki wa shughuli za kisiasa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na kuhakikisha rasilimali za chama zinatumika kwa maslahi mapana ya wanachama.

Semfukwe alidai kuwa kesi hiyo itakapokuja kusikilizwa, viongozi na wanachama watashangaa kubaini namna mali na rasilimali za chama zinavyotumiwa na kufujwa na kikundi cha watu wachache, zikiwamo ruzuku, nyumba, magari, pikipiki na michango ya wanachama pamoja na wahisani kutoka nje ya nchi.

Aidha, ameitaka Mahakama inayosikiliza shauri hilo kulichukua kwa uzito na kulisikiliza kwa wakati mwafaka ili haki iweze kutendeka kwa pande zote.

Kwa upande wake, Said Issa Mohamed alisema aliamua kufungua kesi hiyo kutokana na kile alichodai kuwa kwa sasa hawezi kushiriki vikao vya uongozi wa chama. Alieleza kuwa amekuwa akiyawasilisha madai hayo tangu akiwa madarakani na hata baada ya kuondoka kwenye nafasi ya uongozi, ameendelea kupigania haki za wanachama, hususan wa Zanzibar.

Mohamed, ambaye aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwa takribani miaka 16, alisisitiza kuwa lengo lake ni kuona kunakuwepo usawa na uwazi katika usimamizi wa mali na rasilimali za chama hicho.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  3. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  

    …………………
    ………………………………………………..
    ………………………
    ……………………………………………………………………………………………………………………………….https://www.payathome9.place

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button